JIna la Idara : IDARA YA BIASHARA
Mkuu wa Idara: Ramadhani Mpita
Uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu: 180:1
Idadi ya Vipindi kwa mwalimu kwa juma: 18
Kutakuwa na Idara ya Biashara ambayo itakuwa na masomo ya Commerce na Bookkeeping. Idara itakuwa chini ya mkuu wa Idara ambaye atafanya kazi zifuatazo:
- Kusimamia walimu kutekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa kwenye orodha ya Majukumu ya Mwalimu wa Somo ikiwa ni pamoja na kuliuza somo lake.
- Kusimamia umalizaji wa mihutasari kwa muda uliopangwa kishule.
- Kuhakikisha watoto wenye uelewa wa chini wanasaidiwa na ikibidi kushirikisha Mwalimu Mwandamizi wa Taaluma pamoja na wazazi wa watoto hao na kuweka kukumbuku za juhudi hizo.
- Kuhakikisha kwamba waalimu katika idara yake wanakamilisha majukumu mengine kwa wakati kama yalivyopangwa na kukubalika katika vikao vya taaluma au maelekezo toka juu.
- Kuweka mpango (Action Plan) wa idara na kuhakikisha kwamba unatekelezwa.
- Kutoa taarifa muhimu kwa wakati ili hatua muafaka ziweze kuchukuliwa kwa lengo la kukuza ufanisi na tija.