IDARA: Lugha
Mkuu wa Idara: Mr. Maulid Rajab
Uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu , idadi ya vipindi kwa juma na idadi ya wanafunzi
SN |
Somo |
Mwalimu 1 |
Idadi wanafunzi |
Vipindi |
1 |
Arabic |
1 |
180 |
24 |
2 |
Kiswahili |
1 |
180 |
18 |
3 |
English |
1 |
90 |
18 |
Kutakuwa na Idara ya Lugha ambayo itakuwa na masomo ya Arabic, Kiswahili na English. Idara itakuwa chini ya mkuu wa Idara ambaye atafanya kazi zifuatazo:
- Kusimamia walimu kutekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa kwenye orodha ya Majukumu ya Mwalimu wa Somo ikiwa ni pamoja na kuliuza somo lake.
- Kusimamia umalizaji wa mihutasari kwa muda uliopangwa kishule.
- Kuhakikisha watoto wenye uelewa wa chini wanasaidiwa na ikibidi kushirikisha Mwalimu Mwandamizi wa Taaluma pamoja na wazazi wa watoto hao na kuweka kukumbuku za juhudi hizo.
- Kuhakikisha kwamba waalimu katika idara yake wanakamilisha majukumu mengine kwa wakati kama yalivyopangwa na kukubalika katika vikao vya taaluma au maelekezo toka juu.
- Kuweka mpango (Action Plan) wa idara na kuhakikisha kwamba unatekelezwa.
- Kutoa taarifa muhimu kwa wakati ili hatua muafaka ziweze kuchukuliwa kwa lengo la kukuza ufanisi na tija.
- Kuhakikisha kwamba wanafunzi wanajengewa weledi wa kuwasiliana kwa lugha wanazosisoma hasa Arabic na English.