IDARA: Hisabati na TEHAMA
Mkuu wa Idara: Mr. Ally Halifa Mnzava
Uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu : 90:1
Idadi ya Vipindi kwa mwalimu kwa juma: 18
Idara ya Hisabati na Tehama kama zilivyokuwa idara nyingine itaongozwa na Mkuu wa Idara ambaye atakuwa na majukumu yafuatayo:
- Kusimamia walimu kutekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa kwenye orodha ya Majukumu ya Mwalimu wa Somo ikiwa ni pamoja na kuliuza somo lake bila kuadhiri utekelezaji wa majukumu mengine yaliyoelekezwa.
- Kusimamia walimu kuhakikisha kwamba wanafunzi wanafaulu somo la hisabati ili kuiwezesha shule kuandaa wanasayansi ambao ni hitajio kubwa kwa taifa.
- Kusimamia umalizaji wa mihutasari kwa muda uliopangwa kishule bila kuadhiri umahiri wa wanafunzi katika somo.
- Kuhakikisha watoto wenye uelewa wa chini wanasaidiwa na ikibidi kushirikisha Mwalimu Mwandamizi wa Taaluma pamoja na wazazi wa watoto hao na kuweka kukumbuku za juhudi hizo.
- Kuhakikisha kwamba mifumo ya kompyuta na kielekroniki inafanya ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kuweka mifumo hiyo.
- Kuweka mpango (Action Plan) wa idara na kuhakikisha kwamba unatekelezwa.
- Kutoa taarifa muhimu kwa wakati ili hatua muafaka ziweze kuchukuliwa kwa lengo la kukuza ufanisi na tija.