Teaching, Nurturing & Training
Curriculum in use.
We follow Tanzania national curriculum for the following Subject: Islamic Knowledge, Arabic, English, Kiswahili, Physics, Chemistry, Mathematics, Geography, Biology, History, Civics, Bookkeeping, Commerce and Computer Studies.
We have currently open 2024 for Advanced learning (From Five and Six) with six combination PCB, PCM, EGM, ECA, HGL and HGE
Moral curriculum.
Our school’s main priority is the parenting approach, which gives emphasis on supporting and promoting physical, emotional, social, spiritual and intellectual development of our children by following Islamic principles.
Kila sifa njema ni za Allah pekee Mola mlezi wa viumbe vyote, na Rehma na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad (s.a.w), pamoja na swahaba zake, na wale wote wanaofuata mwenendo wake, mpaka siku ya Kiyama.
Kama tujuavyo, shule ya Ihsan ni shule ya Kiislam ambayo imejidhatiti kuelimisha na kuwanoa vijana katika taaluma ya darasan na nje ya darasa. katika kuyatimiza lengo hilo, tumeweka utaratibu wa kuyafikia malengo hayo kupitia Muhsasari Muhtasari wa somo la Tarbia (malezi) kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne, ambao umetokana na fani zifuatazo:
Katika somo hili, wanafunzi wanajifunza kusoma, kuhifadhi, na kuelewa mafundisho yaliyomo ndani ya Qur’aan ili yawe mwongozo wa maisha yao ya kidini na kijamii.
Hadithi ni maneno, matendo, na idhini za Mtume Muhammad (S.A.W). Katika somo hili, wanafunzi wanajifunza hadithi sahihi za Mtume ambazo ni mwongozo wa kutekeleza mafundisho ya Kiislamu. Hadithi ni chanzo cha pili cha sheria baada ya Qur’aan, na ina umuhimu mkubwa katika kuelekeza maisha ya Muislamu.
Fiqhi ni elimu ya sheria za Kiislamu zinazohusu ibada, muamala (mikataba ya kijamii), ndoa, urithi, na masuala mengine ya kimaisha. Wanafunzi wanajifunza jinsi ya kutekeleza ibada kama vile swala, saumu, zakat, na hajj kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, pamoja na jinsi ya kushughulikia mambo ya kila siku kwa mujibu wa sheria za dini.
Tarekhe ni somo linalohusu historia ya Kiislamu, likiwa na mtazamo wa matukio muhimu ya kidini na kijamii tangu wakati wa Mitume, hususan Mtume Muhammad (S.A.W), mpaka katika zama mbalimbali za Uislamu. Wanafunzi wanajifunza historia ya miji mitakatifu, viongozi wa Kiislamu, na jinsi Uislamu ulivyoenea duniani.
Akh-laaq ni tabia njema na maadili bora ambayo Muislamu anatakiwa kuwa nayo. Katika somo hili, wanafunzi hufundishwa umuhimu wa kuwa na tabia njema kama vile uaminifu, huruma, subira, na heshima kwa wengine. Ni somo la kuimarisha maadili mema katika maisha ya kila siku.
Adhkaaru ni kumbukumbu na nyiradi mbalimbali za kumtaja Mwenyezi Mungu, Dua ni maombi, na Adabu ni adabu njema na jinsi ya kuishi kwa heshima na uangalifu. Katika somo hili, wanafunzi hufundishwa dua mbalimbali kwa nyakati tofauti kama vile wakati wa kusafiri, kulala, na kuamka, pamoja na adabu za kula, kuzungumza, na kuamiliana na watu kwa njia sahihi ya Kiislamu.
Extracurricular activities, Socio-economic services
Beyond the subjects listed above our students are engaged in;
- Karate/ Taekwondo Debating
- Quran studies (Reciting, memorization and meaning competencies)
- Clubs
- Sports and games
- Sacrifice and volunteering in community work
Social and economic services available include reliable transport, water, electricity and dispensaries.